Klabu ya Coastal Union ya mkoani Tanga imehamia mkoani Arusha na itatumia uwanja wa itaufanya uwanja wa Sheik Amri Abedi kuwa uwanja wake wa nyumbani kwenye michezo ya ligi kuu Tanzania bara kipindi chote ambacho uwanja wa Mkwakwani unaendelea kufanyiwa matengenezo. Awali timu hiyo Mabingwa wa ligi kuu ya Tanzania bara mwaka 1988 ilikua inautumia uwanja wa KMC Complex kama uwanja wake wa nyumbani.
Klabu ya Coastal Union ya mkoani Tanga imehamishia makazi yake Jijini Arusha ambapo sasa itautumia uwanja wa Sheikh Amri Abeid kama uwanja wake wa nyumbani na kuachana na KMC Complex uliopo Dar es salaam iliyokua ikiutumia hapo awali.
CCM Mkwakawmi upo kwenye matengenezo hivyo kuilazimu klabu hiyo mabingwa wa Tanzania bara mwaka 1988 inayotokea mkoa wa Tanga kutafuta kiwanja kingine cha nyumbani kwa muda mpaka matengenezo yatakapokamilika.
Sababu kubwa ya kuhamia uwanja huo ni kuthamini mapendekezo ya Wanachama na Mashabiki wa timu hiyo Waliouomba uongozi wa Wagosi wa kaya kuirudisha klabu yao kanda ya kaskizi ili kuwa na uhakika wa kupata alama tatu kutokana na uwezekano wao kuweza kusafiri kwenda kuishangilia.
Coastal imecheza michezo mitano uwanja unaomilikiwa na Manispaa ya Wilaya Kinondoni na kufanikiwa kushinda mchezo mmoja, sare moja na kupoteza michezo mitatu.Mpaka sasa Wana Mangushi Wanashika nafasi ya kumi na tatu msimamo wa ligi kuu Tanzania bara ambayo imesimama kupisha michezo ya timu ya taifa.
Bodi ya ligi inatarajia kutoa ratiba ambayo imefanyiwa marekebisho kutokana na kuwepo kwa michezo ya kufuzu mashindano ya ndani kwa timu za taifa ( CHAN ), kama ratiba itabaki kama ilivyo kwa siku ya Oktoba 18 Wagosi wa Kaya watakuwa wenyeji wa Dodoma Jiji ambapo mechi hiyo itakua ya kwanza Sheikh Amri Abedi Coastal Union kucheza ikiutumia kama uwanja wake wa nyumbani kwenye michezo ya ligi kuu.