Jumapili , 15th Mar , 2015

Kiungo mshambuliaji wa timu ya soka ya Yanga Mrisho Halfan Ngasa hii leo amekuwa nyota na mwiba mkali katika mchezo wa kimataifa wa kombe la shirikisho barani Afrika dhidi ya Platinum FC ya Zimbabwe

Wachezaji wa Yanga wakishangilia moja ya mabao ya mshambuliaji Mrisho Ngasa wa kwanza kushoto

Mshambuliaji hatari wa wawakilishi pekee wa Tanzania katika michuano ya soka barani Afrika Yanga Mrisho Ngasa ameiongoza timu yake kuibuka na ushindi mnono wa mabao 5-1 katika mchezo wa kwanza wa raundi ya pili ya michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika dhidi ya Zimbabwe mchezo uliopigwa katika uwanja wa taifa jijini
Dar es Salaam

Yanga ambayo hii leo ilionyesha kandanda safi tangu mwanzo wa mchezo huo na kuwafurahisha mashabiki wao waliofurika katika uwanja wa taifa walijipatia bao la kwanza kunako dakika ya 26 kwa bao safi lililofungwa na kiungo mkabaji wa timu hiyo Salum Telela huku kunako dakika ya 40 kiungo Haruna Niyonzima akiipatia timu hiyo goli la pili na dakika 5 baadaye sekunde chache kabla ya timu hazijakwenda mapumziko Platinum walijipatia bao lao pekee na lakufutia machozi

Kipindi cha pili Yanga ambayo hii leo ilijidhatiti vilivyo ilipata bao la mapema kunako dakika ya kwanza ya kipindi hicho yaani dakika ya 46 kwa goli safi lililofungwa na mshambuliaji Amis Tambwe

Magoli mengine ya Yanga la nne na la tano yalifungwa na nyota wa mchezo huo wa leo Mrisho Ngasa kunako dakika ya 52 na 90.

Kwa matokeo hayo Yanga imejiweka katika mazingira mazuri ya kufuzu kwa hatua inayofuata kwani inahitaji si ushindi bali sare ya aina yoyote ile au hata ikifungwa mabao yasizidi matatu kwa bila basi itavuzu moja kwa moja na kuitupa nje timu hiyo ya Zimbabwe ambayo watarudiana nayo wiki mbili zijazo huko jijini Harare nchini Zimbabwe.