Jumapili , 11th Dec , 2016

Historia imeandikwa kwenye tasnia ya sanaa nchini ambapo kwa mara ya kwanza tukio la utoaji wa tuzo za #EATVAwards kwa wasanii wa muziki na filamu Afrika Mashariki, limefanyika usiku wa leo katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam.

Tuzo hizo zilizoandaliwa na East Africa Television Ltd, zimekuwa za kwanza Afrika Mashariki, ambapo wasanii mbali mbali wamefanikiwa kujinyakulia tuzo zao.

Tazama orodha nzima ya washindi hapa chini..

Kipengele cha mwanamuziki bora wa kiume

G Nako – 'Original'

Sheta –'Namjua'

Mwana FA – 'Ahsanteni kwa Kuja'

Alikiba – 'Aje' --- MSHINDI

Ben Pol – 'Moyo Mashine'

Mwana muziki bora wa kike

Lilian Mbabazi – 'Yoola'

Ruby – 'Forever'

Lady Jay dee – 'Ndindindi' --- MSHINDI

Linah – 'No stress'

Vanessa Mdee – 'Niroge'

Mwanamuziki bora chipukizi

Manfongo – 'Hainaga ushemeji' --- MSHINDI

Feza Kessy – 'Sanuka'

Rukia Jumbe (Ruky Baby) – 'Mpasuo'

Bright – 'Nitunzie'

Mayunga – 'Nice couple'

Kundi bora la mwaka

Navy kenzo – 'Kamatia chini'--- MSHINDI

Mashauzi Clasic - 'Kismat'

Team Mistari – 'Tuzidi'

Sauti Sol – 'Unconditional bae'

Wakali wao – 'Chozi langu utalilipa'

Video bora ya mwaka

Njogereza – Navio

Namjua – Shetta

Aje – Alikiba -- MSHINDI

Don't Bother – Joh Makini

Ndindindi – Lady Jaydee

Wimbo bora wa mwaka

Don't bother – Joh Makini

Ndindindi - Lady Jayedee

Kamatia chini - Navy Kenzo

Moyo mashine – Ben Pol

Aje – Alikiba --- MSHINDI

Filamu bora ya mwaka

Facebook profile

Safari ya Gwalu --- MSHINDI

Mfadhili wangu

Hii ni laana

Nimekosea wapi

Muigizaji bora wa kiume

Meya Shabani Khamisi

Salim Ahmed (Gabo) --- MSHINDI

Daudi Machael (Duma)

Doto Hussein Matotola

Said Mkukila

Muigizaji bora wa kike

Chuchu Hansy --- MSHINDI

Rachel Bithulo

Frida Kajala Masanja

Khadija Ally

TUZO YA HESHIMA

DJ Maarufu bongo Boniventure Kilossa (Dj Bonny Love) ndiye mtu aliyepewa tuzo maalum ya heshima, akitambuliwa kutokana na mchango wake kwenye tasnia ya sanaa hapa nchini

Tags: