Tangu kuanza kwa matumizi ya gesi katika vyombo vya moto jijini dar es salaam idadi ya watumiaji inaelezwa kuongezeka hii ni kutokana na faida za kibiashara na kiuchumi ambazo watumiaji hao wamezitaja.
Takribani masaa matatu hadi manne ndiyo muda wa kukaa foleni kusubiri kujaza gesi hii imesabisha baadhi kutokuhimili kungoja, na hapa serikali inaombwa kuongeza vituo zaidi ili visaidie kuhudumia idadi hiyo ya watumiaji kwani kwa sasa ni vituo vitatu pekee vinavyotoa huduma.
Kwa upande wa mtaalamu wa uchumi ameeleza faida zinazotokana na matumizi hayo hasa watumiaji kwa ajili ya vyombo vya usafiri vya kibiashara, huku faida kubwa ikiwa inamlenga mwananchi mmoja.