Jumanne , 28th Jul , 2020

Rais wa Tanzania Dk. John Magufuli amridhia uwanja wa taifa kuitwa jina la Mkapa kufuatia kuwapo kwa maombi ya wadau wengi wa michezo kutaka uwanja huo uitwe jina la Benjamin Mkapa tangu kutokea kifo chake 23/07/2020 mwaka huu Jijini Dar es Salaam.

Muonekano wa Uwanja wa Taifa ambao kwa sasa utaitwa Mkapa Stadium Picha na maktaba.

Rais wa Tanzania Dk. John Magufuli amridhia uwanja wa taifa kuitwa jina la Mkapa kufuatia kuwapo kwa maombi ya wadau wengi wa michezo kutaka uwanja huo uitwe jina la Benjamin Mkapa tangu kutokea kifo chake 23/07/2020 mwaka huu Jijini Dar es Salaam.

Akihutubia taifa katika siku ya kitaifa ya kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Hayati Mkapa rais Dk. Magufuli amesema kwamba Mzee Mkapa alitoa mchango wake katika kila sekta ya michezo na sanaa, na Watanzania hawatomsahau kwa kujenga uwanja huo wa taifa.

“Mzee Mkapa aliujenga uwanja mkubwa wa michezo,kwa sasa wengi wanataka uwanja uitwe ‘Mkapa Stadium”

Dk. Magufuli amesema kwamba amekuwa akipokea meseji nyingi zikitaka uwanja huo kuitwa wa Benjamin Mkapa, anafahamu Mzee Mkapa hakuwa akipenda vitu vingi kuitwa jina lake lakini kwa kuwa ameshalala hapa sasa, anatamka uwanja huo sasa kuitwa rasmi wa Mkapa.

“Mkapa amefanya mengi kwenye sekta ya michezo, na ni kwasababu aliipenda michezo pia naambiwa alikuwa shabiki wa Yanga ingawa sikuwahi kumsikia akisema hadharani..Mzee Kikwete ananiambia hapa kweli alikuwa Yanga maana na Kikwete ni shabiki wa Yanga, sijui Mwinyi timu gani!”