Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Simba, Yanga zampoteza kiungo

Jumatano , 23rd Aug , 2017

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limemfungia kiungo wa Yanga Pius Buswita mwaka mmoja kwa kosa la kusaini kwa wakati mmoja mikataba na timu mbili tofauti yaani Simba na Yanga akitokea Mbao FC.

Nembo ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

Hayo yameweka wazi baada ya kikao cha  Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) inayoongozwa na Wakili Richard Sinamtwa, ambayo ilikutana Agosti 20 mwaka huu Jijini Dar es Salaam kupitia usajili wa majina ya klabu 40 uliyofanywa katika kipindi cha usajili.

Kamati hiyo ilibaini kwamba mchezaji huyo aliyechezea Mbao FC ya Mwanza msimu uliopita Pius, amevunja Kanuni ya 66 ya usajili Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo inaelekeza adhabu ya kufungiwa mwaka mmoja. 

Katika hatua nyingine, Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imepitisha jina la Kidao Wilfred kuwa Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho hilo.

Kidao ambaye ni mchezaji wa zamani wa Taifa Stars ambaye pia Mwenyekiti wa Chama cha Makocha Tanzania (TAFCA), ameteuliwa rasmi jana Agosti 22, 2017 na Kamati ya Utendaji ya TFF

HABARI ZAIDI

Baadhi ya Wakazi wa Kata ya Madanga Mkoani Tanga

Wagoma kubeba mimba kwa kukosa huduma za afya

Mkuu wa mkoa wa Songwe Daniel Chongolo

Wanafunzi 194 washika mimba ndani ya mwezi mmoja

Mabaki ya gari aina ya Noah iliyopata ajali Morogoro

Ajali yachukua uhai wa watu saba Morogoro

Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba

Wawekezaji wawekeze sekta za uzalishaji - Nchemba

Muonekano wa Kiburugwa ambako Nyumba zaidi ya Tisa Zimebomolewa na Maporomoko ya Tope

Maporomoko ya udongo yasomba nyumba 9 Mbagala

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko

Serikali yaipongeza Red Cross

Waziri wa TAMISEMI Mohamed Mchengerwa

Aonya wanaochangia watumishi kutopanda madaraja