Alhamisi , 21st Jan , 2021

Klabu ya Manchester United ‘Mashetani wekundu’ wamefanikiwa kurejea kileleni mwa msimamo wa ligi kuu England ‘EPL’ baada ya kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Fulham usiku wa kuamkia leo tarehe 21 Januari 2021 na kufikisha jumla ya alama 40.

Matukio mbalimbali kwenye mchezo wa Fulham dhidi ya Manchester United kwenye mchezo wa usiku wa jana ambapo umemalizika kwa Manchester kushinda mabao 2-1.

Fulham ndiyo iliyokuwa ya kwanza kupata bao, lililofungwa na winga wake Ademelo Lookman aliyefunga dakika ya tano na Edinson Cavani kuisawazishia Manchester United dakika ya 21 kabla ya Paul Pogba kufunga bao safi na la ushindi dakika ya 65.

Baada ya ushindi huo, Manchester United imefikisha jumla ya alama 40 na kushika usukani wa EPL licha ya kuwa na michezo 19 mmoja mbele ya Manchester City aliyefikisha alama 38 baada ya kuifunga Aston Villa mabao 2-0 kwenye dimba la Etihad usiku wa jana.

Leicester City ambayo wikiendi iliyopita imeifunga Chelsea mabao 2-0 kwenye dimba la king power, ipo nafasi ya tatu ikiwa na alama sawa na Manchester City, alama 38 kswenye michezo 19 mchezo mmoja mbele ya Manchester City.

(Kiungo wa Manchester United, Paul Pogba ()katikati kwenye picha) akishangilia baada ya kufunga bao la ushindi dhidi ya Fulham usiku wa jana.)

Manchester United amekwaa kileleni mwa msimamo EPL kwa kishindo kwani ameweka rekodi kali ya kushinda michezo 7 ambayo alitanguliwa kufungwa, rekodi iliyowekwa msimu wa mwaka 2001-02 na Newcastle iliyoshinda michezo 10 iliyotanguliwa kufungwa.

Ni mara ya pili Manchester United kuweka rekodi ya namna hiyo, kwani msimu wa mwaka 2012-13 ambao walikuwa mabingwa wa EPL, kwa mara ya mwisho walishinda michezo 9 waliyotanguliwa kufunga.

Rekodi nyingine ya kibabe waliyoiweka Manchester United ni  rekodi ya kufikisha michezo 17 bila kufungwa kwenye viwanja vya ugenini, ikishinda michezo 13 na kutoka sare michezo 4 na kuifikia rekodi waliyoiweka msimu wa mwaka 1999 ambao walitwaa ‘Treble’.