Mtaalamu wa Afya ya kinywa ameeleza kuwa watu wengi wamekuwa na nadharia ya kwenda kung'oa meno bila kwenda kupata tiba
Mtaalamu wa Afya ya kinywa ameeleza kuwa watu wengi wamekuwa na nadharia ya kwenda kung'oa meno bila kwenda kupata tiba huku wengine hawana elimu ya kufanya usafi wa kinywa na hapa anaeleza.
"Sio kila jino nila kung'oa ndomana tunazidi kutoa elimu kwa watu ili kujua kama jino lililotoboka linatakiwa kutolewa, mara chache kama litahitajika kutibiwa zaidi na kuna namna yakufanya usafi kama hapa kuna nmna yakusafisha meno ili kuondo uchafu wote". Amesema Dkt. Balbina Beda, Daktari wa Afya ya kinywa na Meno - Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala.
Baadhi ya wananchi wameeleza kuwa mtindo wa maisha wanayoishi imekuwa ikichangia kuharibika kwa meno na kutofanya usafi wa kinywa mara kwa mara pamoja na kutopata ushauri kutoka kwa wataalamu ili kuweza kujua njia ipi sahihi ya kulinda afya ya kinywa.
"Watu wengine ynakuta wanafanya usafi wa kinywa vizuri ila shida inakuja pale mtu anapokuwa na mwenza anakwenda kufyonza vitu ambavyo sio hali inayosababisha kupata magonjwa ya kinywa". Amesema Abubakar Ndembo, Mkazi wa Kivule Dar es Salaam
"Tumekuwa tukiona mtu anakula sana vitu vya sukari nyingi huku kufanya usafi hawafanyi vizuri ndo mana unakuta mtu meno yanaoza inampelekea kwenda kungoa meno". Amesema Danford Mkumbo Isack, Mkazi wa Ubungo Dar es Salaam.
"Maranyingi watu huwa hatuna uelewa ule wa jinsi ya kupiga mswaki maranyingi mtu unashauriwa ukiamka piga mswaki na ukila vyakula piga mswaki lakini watu huwa hatuna huu uelewa". Amemsema Razak Lusinga, Mkazi wa Magomeni mikumi Dar es Salaam.
Kwamujibu wa taarifa ya Shirika la Afya Duniani iliyotolewa mwaka 2024 inaeleza kuwa magonjwa ya kinywa, kama vile kuoza kwa meno, magonjwa ya fizi, na upotevu wa meno, bado yanaenea katika Kanda ya Afrika na kuathiri karibu asilimia 44 ya watu.