Alhamisi , 27th Nov , 2025

Hili ndilo shambulio baya zaidi dhidi ya walinzi wa kitaifa tangu Rais Trump aanze kuviagiza vikosi hivyo kushika doria katika maeneo mbalimbali nchini humo tangu arejee tena madarakani mwezi Januari. 

Shambulio la risasi karibu na Ikulu ya Marekani usiku wa kuamkia leo Alhamisi Novemba 27 limejeruhi walinzi wawili wa jeshi la kitaifa la Marekani na kuwaacha katika hali mahututi.

Katika taarifa yake, Rais wa Marekani Donald Trump amelitaja shambulio hilo kuwa ni la kigaidi na ambalo limechochewa na chuki. Trump amesema mtu aliyewashambulia walinzi hao ni mhamiaji raia wa Afghanistan aliyeingia nchini Marekani kinyume na sheria mwaka wa 2021.

Kwa mujibu wa Rais Trump, serikali yake itaanzisha oparesheni kubwa ya kuangazia namna kila wageni walivyoingia nchini Marekani wakati wa uongozi wa mtangulizi wake Joe Biden.

Tayari mamlaka imethibitisha kumkamata mshambuliaji huyo ambaye aliripotiwa kujeruhiwa kwenye makabiliano na maofisa wa usalama wakati wa tukio hilo la shambulio la kushtukiza.

Wakati wa shambulio Rais Trump alikuwa katika Mji wa Florida, hatua iliyopelekea kusitishwa kwa shughuli za kawaida katika Mji huo kwa muda.

Hili ndilo shambulio baya zaidi dhidi ya walinzi wa kitaifa tangu Rais Trump aanze kuviagiza vikosi hivyo kushika doria katika maeneo mbalimbali nchini humo tangu arejee tena madarakani mwezi Januari.