Jumapili , 5th Jan , 2025

Mtoto mwenye umri wa miaka nane mkazi wa Kata ya kalangalala Manispaa ya Geita Mkoani Geita anadaiwa kubakwa na kijana mmoja ambae ni jirani yake baada ya mtoto huyo kwenda kutazama TV kwenye chumba cha mtuhumiwa huyo.

Mtoto abakwa akiangalia Tv kwa jirani

Akizungumza kwa masikitiko  babu wa mtoto huyo anasema familia ilianza kuhisi kuna jambo lisilo la kawaida baada ya mtoto huyo kuanza kutembea kwa shida walipomhoji alikiri kufanyiwa ukatili na kijana huyo.

“Yule mtoto nilivyombana akaniambia ni kweli aliniingiza ndani akaanza kunichezea akanivulisha sketi kwakweli inauma sana ninaomba serikali ichukue mkondo wake” Babu wa Mtoto huyo

“Mimi nilianza kumwona mtoto huyo anatembea mguu mmoja huku mwingine kule nikamuuliza umefanyaje akasema nimechomwa mti nikasema wewe unadanganya sema ukweli akakiri kwamba amebakwa na kijana ambaye ni jirani yao maana wakati huo kalikuwa kamejifunga kitenge mabega hivi” Mkazi wa Lwenge

“Tulipokuwa tunamuuliza alikuwa anaogopa kusema lakini tulivyotaka kumchapa kwamba aseme ukweli ndo alisema kuwa kweli amefanyiwa kitendo hicho”Catherine Boniface, Balozi wa mtaa wa Lwenge

“Tulivyomuhoji mama yake na Yule mtoto alisema watoto wale waga wanaenda kuangalia TV Mule na mtuhumiwa tulivyomuhoji naye alisema ni kweli watoto waga wanakuwa wanaenda kuangalia TV Kwake”Simon Marijani, Polisi jamii mtaa wa Lwenge

Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya mji wa Geita Yohana Mlole amethibitisha kumpokea mtoto huyo na kumfanyia vipimo ambapo baada ya tukio hilo mtuhumiwa huyo alichukuliwa na jeshi la polisi kwaajili ya mahojiano na uchunguzi zaidi.

“Baada ya kumfanyia uchunguzi yapo mambo tuliyoyagundua kuusu Yule ila kutokana na kumhifadhi mgonjwa na usiri siwezi kuyazungumza moja kwa moja lakini alifika na tulimfanyia uchunguzi”Dkt Yohana Mlole, Kaimu mganga mfawidhi Hospitali ya Mji Geita.