Jumatano , 26th Aug , 2015

Timu ya Majimaji ya Songea mkoani Ruvuma imewasajili wachezaji wawili wa Azam FC beki Ismail Gambo ‘Kussi’ na kiungo Omary Wayne kwa mkopo wa muda mrefu wa msimu.

Ismail Gambo ‘Kussi' (Kushoto ) na Omary Wayne (Kulia) waliochukulia na Majimaji kwa mkopo wakitokea Azam Fc

Wawili hao matunda ya "Academy" ya mabingwa hao wa Afrika Mashariki na kati tayari wamesafiri kwenda Songea kujiunga na Majimaji iliyorejea ligi kuu ya soka Tanzania Bara msimu huu.

Wawili hao wanafanya idadi ya wachezaji watatu ndani ya wiki moja kutolewa kwa mkopo Azam FC, baada ya winga Joseph Kimwaga kupelekwa Simba SC wiki hii.