Alhamisi , 18th Jul , 2024

Nyota Mmarekani Tyrese Haliburton amesema kushinda medali ya dhahabu ya michezo ya Olimpiki ya Paris 2024 itakayofanyika nchini Ufaransa ni kitu cha kujivunia kama kushinda taji la ubingwa wa Ligi ya kikapu ya Marekani .

Haliburton mwenye umri wa miaka 24 amesema nafikiria kushinda medali ya dhahabu kwenye michezo ni kitu cha kujivunia kwenye mchezo wowote pamoja na kushinda taji la NBA kwangu nahisi ni vitu vikubwa kuliko vitu vingine binafsi.

Tyrese Haliburton anayeichezea timu ya Indiana Pacers ni miongoni  mwa nyota watakaoiwakilishi  Marekani kwenye michuano ya kikapu sambamba na nyota kama Steph Curry,LeBron James,Joel Embid,Kevin Durant huku timu hiyo imeshinda mara 16 medali za dhahabu kwenye michezo ya Olimpiki