Jumanne , 25th Mar , 2014

Baraza la michezo Tanzania BMT limevitaka vyama vyote vya michezo ambavyo vitatoa wawakilishi katika michuano ya jumuiya ya madola itakayofanyika jijini Grascow nchini Scotland, kuwasilisha majina na kumbukumbu za wachezaji wao mapema.

BMT imesema wanapaswa kuwasilisha hivyo vitu mapema katika ofisi za kamati ya olimpiki Tanzania TOC kwaajili ya kushughulikiwa taratibu za safari

Afisa michezo wa BMT Richard Mganga amesema kuwa kumekua na kusuasua kwa vyama hivyo kupeleka majina hayo TOC na ikumbukwe kuna ofa ilitolewa na Wizara ya mambo ya nje kwa baadhi ya wachezaji kutoka vyama hivyo wapatiwe nafasi kwenda nje ya nchi kufanya maandalizi zaidi kabla ya michuano hiyo ya jumuiya ya madola kuanza mwezi julai mwaka huu.