Jumanne , 21st Apr , 2026

 Arne Slot anatarajiwa kuendelea kuwa meneja wa Liverpool kwa msimu ujao Licha ya kuwa na mwanzo mbaya wa msimu huu uliowafanya kupoteza alama nyingi na kutoka kwenye mbio  za ubingwa.

 Arne Slot

Liverpool wamepoteza michezo 10 ya Ligi Kuu hadi sasa msimu huu, ambayo ni mingi zaidi tangu msimu wa 2015/16 ambao ulianza na Brendan Rodgers na kumalizika na mtangulizi wa Slot, Jürgen Klopp.

Slot atakuwa na kazi kubwa msimu huu wa joto huku Andy Robertson na Mohamed Salah Salah wakiwa wachezaji wawili muhimu ambao watahitaji kubadilishwa. 
Kocha huyo pia atatafuta kupata mbadala wa safu yake ya ushambuliaji inayosumbuliwa na majeraha wakiwakosa wachezaji kama Hugo Ekitike na Alexander Isak

Tangu achukue nafasi ya Anfield, Slot amesimamia michezo 108, akishinda 65, sare 17, na kupoteza 26 katika mashindano yote - huku mechi 17 kati ya hizo zikipigwa msimu huu.