
Picha ya Kanye West kushoto kulia ni Cardi B

Moja ya jengo likiwaka moto Kariakoo
Waliokamatwa kwa wizi wa mifugo

Meneja Mwandamizi wa GGML anayeshughulikia mahusiano ya jamii, Gilbert Mworia akimpatia maelezo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman kuhusu shughuli zinazofanywa na kampuni hiyo katika sekta ya madini. Makamu huyo alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya kufunga maonesho hayo.

Wananchi waliotembelea Maonesho ya sita ya teknolojia ya Madini Geita jana wakisubiri katika banda la Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Geita ili kujiandikisha na kupata huduma za uchunguzi wa saratani na elimu kutoka kwa wataalam wa tiba. Huduma hiyo inayotolewa bila malipo na Hospitali ya Rufaa ya Geita kwa kushirikiana na Kampuni ya Geita Gold Mining Company Limited (GGML), inajumuisha uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi, matiti na tezi dume.

Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (katikati), akisikiliza maelezo kutoka kwa mhandisi wa majengo wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), wakati alipotembelea kukagua ujenzi wa miradi inayoendelea katika Chuo hicho, jijini Arusha.

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt.Doto Biteko akizungumza na wananchi katika Kijiji cha Ntanga wilayani Ngara Mkoa wa Kagera wakati alipofika kuwasha umeme kwenye kijiji hicho.