Jumapili , 1st Oct , 2023

Baada ya watumiaji wa toleo jipya la simu aina ya Iphone ''Iphone 15" kulalamika kuhusiana na changamoto ya simu zao kupata joto pindi wanapotumia, 

 

Kampuni ambayo ndiyo watengenezaji wa simu hizo ''Apple Inc'' wametolea ufafanuzi kwa kusema ni changamoto iliyomo ndani ya toleo jipya la mfumo endeshi uliyoboreshwa hivi karibuni

Mfumo huo ambao unafahamika kama ''IOS'' ikiwa na maana ''iPhone operating system'' ni wa 17 katika matoleo yake na umeonekana kuleta matokeo ya haraka kwenye kudhihirisha udhaifu wa mfumo huo,

Kwa sababu Iphone 15 ndiyo toleo ambalo lilikuja moja kwa moja na mfumo huo ukiachana na watumiaji wa matoleo mengine ya simu ambao walikuwa wanawezeshwa kufikia maboresho hayo.

Hii inakuwa si mara ya kwanza kwa kampuni hiyo kutambulisha mfumo wa ''IOS'' ambao umekuwa changamoto kwa watumiaji wa simu aina ya ''iPhone'', 

Kwani mwaka 2010 walikumbana na skendo kubwa ambayo iliwalazimu kulipa mabilioni ya pesa kama sehemu ya fidia kwa hasara iliyotokea.

Kwa mwaka 2010 kampuni ya ''Apple Inc'' ilitambulisha mfumo wa ''iOS 10.2.1'' ambao ulileta changamoto ya kuharibu betri za watumiaji waliojaribu kutumia mfumo huu hali iliyopelekea kampuni hiyo kulipa fidia kwa watu zaidi ya milioni 3 

Kwa mujibu wa wavuti wa (AugustMan) unaandika kwa kila aliyepata changamoto kampuni ililazimika kulipa si chini ya 753,110 kwa pesa ya kitanzania kama fidia.

Picha : http://ISP.page