Jumapili , 1st Oct , 2023

Kikosi cha Simba SC kimevuka hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) kwa ushindi wa jumla mabao 3-3 ikipata faida ya kufunga mabao mawili ugenini Zambia na leo ikitoka sare 1-1 nyumbani Azam Complex.

Bao la Dynamos limefungwa na Andy Boyeli dakika ya 16 na Kondwani Chiboni alijifunga dakika ya 68 na ubao kusoma 1-1, Simba inaungana na Yanga ambayo ilifuzu jana hatua ya makundi.

kikosi Kamili kilivyopangwa

Ayoub Lakred (36), Shomari Kapombe (12), Mohamed Hussein (15), Kennedy Juma (26), Che Fondoh Malone (20), Mzamiru Yassin (19), Fabrice Ngoma (6), Clatous Chama (17), Jean Baleke (4), Said Ntibazonkiza (10), Kibu Denis (38).

Wachezaji wa Akiba:

Ally Salim (1), Israel Patrick (5), Hussein Kazi (16), Abdallah Hamis (13), Sadio Kanoute (8), Willy Onana (7), John Bocco (22), Moses Phiri (25), Shaban Chilunda (27).