Jumapili , 1st Oct , 2023

Watu watatu akiwemo mfanyakazi wa shamba la mifugo la serikali Mabuki wilayani Misungwi mkoani Mwanza wanashikiliwa na jeshi la polisi wilayani humo kwa tuhuma za wizi wa ng'ombe tisa za mradi wa vijana wa unenepeshaji wa BBT.

Waliokamatwa kwa wizi wa mifugo

Mkuu wa wilaya ya Misungwi Paul Chacha, amewataja vijana hao kuwa ni Daud Msobi, Shileta Paul na Boniphace Kileleju huku akiagiza vijana wengine 60 wanaoshiriki mradi huo kuhojiwa.

Kwa upande wake meneja wa BBT kampasi ya Mabuki Jacob Chacha, ameeleza kushtushwa na tukio hilo la wizi la wa ng'ombe na kuomba jeshi la polisi kuendelea kuimarisha ulinzi.