Belarus imewaachilia huru wafungwa 123 wa nchi mbalimbali kufuatia mazungumzo baina ya wa Belarus Alexander Lukashenko na Marekani, jana Jumamosi, Desemba 13.
Miongoni mwa walioachiwa ni mwanaharakati Ales Bialiatski, mpokeaji mwenza wa Tuzo ya Amani ya Nobel ya 2022, na kiongozi wa upinzani Maria Kolesnikova ambaye alikuwa gerezani tangu mwezi Septemba 2020 baada ya upinzani wake mkubwa dhidi ya jaribio la kumtimua katika nchi yake.
Alihukumiwa kifungo cha miaka 11 jela mwaka 2021, akitumia zaidi ya miaka minne jela, ikiwa ni pamoja na mwaka mmoja na nusu katika kifungo cha upweke, bila kuwasiliana na ndugu, jamaa na marafiki zake.
Bialiatski, ambaye ni mpokeaji mwenza wa Tuzo ya Sakharov ni mmoja wa watu mashuhuri walioshiriki katika harakati za maandamano ya mwaka 2020 dhidi ya Rais wa taifa hilo, Alexander Lukashenko.
Kuachiliwa kwake kunakuja siku moja baada ya ziara ya mjumbe wa Donald Trump nchini Belarus, ambaye alitangaza kuondolewa kwa vikwazo vya Marekani dhidi ya potasiamu inayozalishwa na nchi hii ya Ulaya Mashariki, mshirika wa karibu wa Urusi.
Belarus ni mzalishaji mkuu wa potasiamu, inayotumika hasa katika utengenezaji wa mbolea. Hata hivyo, sekta hiyo na nyingine ambazo ni muhimu katika uchumi wa nchi hiyo zinakabiliwa na vikwazo vikali vya Marekani na Ulaya kutokana na ukandamizaji dhidi ya upinzani nchini Belarus na uungaji mkono wa Minsk kwa mashambulizi ya Urusi nchini Ukraine yaliyoanzishwa mwaka wa 2022.
Katika miezi ya hivi karibuni, Donald Trump ameihimiza Belarus kuwaachilia mamia ya wafungwa wa kisiasa nchini humo, na Rais wa Belarus Alexander Lukashenko, aliye madarakani kwa zaidi ya miaka 30, aliwasamehe watu kadhaa.
Tayari Washington imeondoa vikwazo kwa kiasi fulani dhidi ya shirika la ndege la Belarus la Belavia, ikiiruhusu kudumisha na kununua vipuri vya ndege zake, ikiwa ni pamoja na ndege za Boeing.


