Jumanne , 18th Jul , 2023

Mwili wa mwanamitandao nchini Nigeria Augusta Osedion (21), umekutwa kwenye nyumba aliyokuwa akiishi mpenzi wake aitwaye Killa Boi (26), ambaye naye kupitia ukurasa wake wa Instagram amekiri kumchoma kisu mpenzi wake huyo kufuatia ugomvi wa mapenzi waliokuwa nao.

Kushoto ni Benjamin Best maarufu kama Killa Boi na kulia ni aliyekuwa mpenzi wake

Kupitia Insta Story yake Killa Boi amesema alimchoma na kisu kwa bahati mbaya na kusema anajiona ni mwenye hatia na kwamba hafai kuendelea kuishi tena duniani kwa kusababisha kifo cha mpenzi wake aliyekuwa akimpenda sana.

Kijana huyo ameongeza kuwa alitamani hata kuurudisha muda nyuma na pengine angekuwa ameachana na mahusiano hayo ambayo alidai yalikuwa ni sumu kwake na kueleza ni kwa namna gani amemkosea Mungu wake, Mama yake na hata ndugu wengine huku akisema hana hatia katika hilo.

Aidha taarifa zinadai kwamba mwili wa binti huyo umekutwa ukiwa umenyofolewa baadhi ya viungo vya mwili ikiwemo sehemu za siri, matiti na macho.