Jumatatu , 5th Jan , 2015

Msanii wa filamu Wastara Juma, ambaye ni mjane wa aliyekuwa staa wa filamu mahiri nchini, Marehemu Sajuki Juma Kilowoko, ameweka wazi kuwa baada ya kufariki kwa mumewe, hakuna manufaa yoyote ambayo yanaendelea kupatikana katika filamu.

muigizaji wa filamu nchini Tanzania Wastara

Wastara ameongezea kusema kuwa hakuna mafanikio ambayo yanaendelea kupatikana ama yanatarajiwa kupatikana kwake na familia kutokana na mfumo wa biashara hiyo ya filamu.

Wastara amesema kuwa, kazi ambazo Marehemu ameziacha na nyingine nyingi za filamu huuzwa kwa wasambazaji na hakimiliki zake zote na hivyo kuendelea kusambazwa miaka na miaka bila msanii kufaidika na chochote kama ilivyo kwa kazi za Marehemu Sajuki.