Alhamisi , 28th Jan , 2016

Rapa Rabbit kutoka nchini Kenya amemshambulia Juliani, akimtaka aache kutumia jina lake kujitengenezea umaarufu, ikiwa ni baada ya Juliani kuwatangaza Rabbit na Khaligraph kumkimbia kushiriki katika show ya kumsaka mfalme wa game ya muziki Kenya.

Rabbit ameeleza kuwa, amekuwa akimsikiliza Juliani toka akiwa shule akiwa kama moja ya wasanii waliomvuta katika sanaa, akifafanua pia sababu za yeye kutokushiriki katika onesho la msanii huyo la Who is King lililokuwa lifanyike mwishoni mwa wiki hii, ni kutokana na dau lake kutofikiwa.

Rabbit amemtaka Juliani ambaye ni kaka yake kimuziki kuacha kitendo hicho cha kutengeneza ligi mitandaoni, akiwataka wapambane kwa kutumia kazi, binafsi akiwa amejikita studio muda wake mwingi kujaribu kuinyanyua game ya muziki Kenya.