Jumamosi , 30th Mei , 2015

Mkuu wa vipindi wa East Afrika Radio, Nasser Kingu ametangaza ujio wa Planet Bongo mpya kabisa ambayo itaanza kuruka katikati ya wiki kuanzia tarehe 1 mwezi ujao.

Historia mpya imeandikwa katika tasnia ya burudani Tanzania siku ya leo ambapo kupitia show ya Planet Bongo iliyokuwa ikitambulika kuwa ni ya mwisho kabisa kufanyika, Mkuu wa vipindi wa East Afrika Radio, Nasser Kingu ametangaza ujio wa Planet Bongo mpya kabisa ambayo itaanza kuruka katikati ya wiki kuanzia tarehe 1 mwezi ujao.

Kupitia show ya radio ya #PlanetBongoYaMwisho leo iliyokuwa ikionekana moja kwa moja pia kupitia EATV, ikiendeshwa na mtangazaji legendary, Salama Jabir pamoja na DJ Big Man Kim, ikiwa na ugeni mzito wa mastaa kibao ndani, Professa Jay, Mwana FA, Mwasiti, Jay Moe na Enica kati ya wengine Kingu amesema huu ni mkakati wa kuongeza nafasi zaidi kwa muziki wa nyumbani kukua, kuongeza burudani zaidi ikizingatiwa show hii itakuwa ikiruka kuanzia saa 7 mpaka saa 10 jioni.

Vilevile Nasser Kingu akatumia nafasi hiyo kutambulisha timu ambayo itakuwa ikishambulia kwa upande wa kukufikishia burudani katika Planet Bongo Mpya, akiwepo mtangazaji Abdallah Khamis Ambua aka Dullah, Anna Peter na Kenedy The Remedy, DJ Ommy Crazy Mtu Mbaya, mtoto Mrembo DJ Sinorita, na mkali wao mwenyewe DJ Summer.

eNewz ambao tumefuatilia kwa makini sana mwanzo hadi mwisho wa tukio hili la kihistoria, tukawavuta chemba masterling wa TeamPlanet Bongo Mpya, Dulla, Anna na vile vile Kenedy ambao wameahidi makubwa kuhusiana na jukumu lao jipya.

Offcourse kwa eNergy hii, Planet Bongo itakuwa ni Boonge moja la show, na kwa wewe shabiki unaweza kueleza kwa njia ya mtandao moments unazokumbuka, na unazozikubali kutoka show hii, na kwenda nayo sawa ukitumia hashtag #PLANETBONGO, kesho utapata nafasi ya kuwasikia mastaa mbali mbali ambao tumeongea nao, pia mashabiki kuhusiana ujio huu mpya wa PB kupitia eNews ya EATV