Jumatano , 30th Apr , 2014

Rapa mkali kabisa kutoka nchini Uganda, GNL Zamba yupo katika wakati mgumu hasa baada ya taarifa kuvuja kuwa anadaiwa kiasi cha shilingi mil. 10 za Uganda, kitita ambacho alikopa kwa ajili ya mandalizi ya onyesho lake la Ceazar ambalo halikufanyika.

GNL Zamba

Taarifa mpya kuhusiana na sakata hili zinaeleza kuwa, GNL amekwishapewa onyo na mdai wake ambaye amefahamika kwa jina Darius, kulipa pesa hizo kabla hajamchukulia hatua, ambapo sasa rapa huyu yupo katika jitihada za kuzichanga ili alipe deni hili.

GNL alichukua pesa hizi mapema mwezi wa pili, na kwa mujibu wa ripoti, baada ya onyesho lake la Aprili 18 kuzuiwa kufanyika, amekuwa na wakati mgumu kurudisha pesa za watu.