Jumatano , 19th Mar , 2014

Msanii wa muziki Uganda, Geosteady ambaye hivi karibuni amemaliza kesi iliyokuwa ikimkabili kwa kunakili kazi ya muziki ya marehemu Elly Wamala bila idhini na kuifanya yake, atazindua albam yake mpya, ambayo ina kazi hii ndani yake.

Geosteady ambaye alikuwa akidaiwa fidia ya shilingi za Uganda milioni 40 kwa kosa hilo, baada ya kukaa chini ya ulinzi kwa muda, amewashangaza wengi kwa kuamua kuendelea mbele na kutumia kazi hii, wakati ambapo inafahamika kuwa hakuna malipo yoyote ya fidia yaliyofanyika.

Hata hivyo, taarifa za chini chini zinasema kuwa, msanii huyu aliachiwa na polisi baada ya kufikia makubaliano fulani na binti wa marehemu Wamala.