Jumanne , 22nd Sep , 2015

Mgombea urais kupitia Chama cha Mapinduzi Mh. Dkt. John Magufuli amewataka viongozi waliohamia upinzani kuwaomba radhi wananchi kwa kutowaletea maendeleo wakati wa uongozi wao.

Mgombea Urais Kupitia Chama cha Mapinduzi Mh. Dkt. John Magufuli

Mh. Magufuli amesema hayo wilayani Muleba Mkoani Kagera ambapo amesema kuwa viongozi hao wanaposimama majukwaani na kusema kuwa serikali haikufanya lolote ni sawa na kuwalaghai wananchi na kutaka kujipima kwa utendaji wao kazi wakiwa madarakani.

Aidha ameongeza kuwa endapo watanzania watampa ridhaa ya kuingia madarakani ataimarisha zao la Kawaha kwa mkoa wa Kagera ili kuendelea kuwa zao kuu la biashara.

Dkt. Magufuli amesema hayo jana mkoani Kagera katika ziara yake ya kampeni na kusema kuwa moja ya mikakati yake ni kupunguza rundo la kodi kwa wakulima ili wakulima waweze kuuza mazao yao kwa bei ya juu.