Jumatatu , 30th Dec , 2019

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Dodoma Dkt. Ernest Ibenzi ameeleza kupokea miili ya watu 6 ambao wamefariki Dunia katika ajali iliyotokea usiku wa kuamkia leo, katika eneo la Kisasa jijini Dodoma, iliyohusisha gari aina ya Toyota Coaster na Lori.

Jiji la Dodoma

Akizungumza kwa njia ya simu na EATV na EA Radio Digital Mganga Mfawidhi Dr. Ernest amesema majira ya saa 5 usiku wa Disemba 29 wamepokea watu 16 huku sita kati yao wakiwa wameshafariki tayari

"Ni kweli kuna ajali imetokea usiku wa kuamkia leo, ikihusisha Lori na Coaster na Hospitali ya Mkoa tulipokea miili ya watu 16, na kati yao 6 ikiwa imeashakufa tayari, lakini pia bado hatujaitambua."

"Hivi karibuni tutawapa taarifa zaidi kuhusiana na majina ya marehemu" ameongeza Dkt. Ernesti