Selemani Jafo - Naibu Waziri TAMISEMI
Naibu Waziri Jafo ametoa kauli hiyo mjini Dodoma wakati akifungua mafunzo ya siku tatu ya sheria mpya ya manunuzi kwa wajumbe wa bodi za manunuzi kutoka taasisi mbalimbali za serikali na za umma mjini Dodoma kwa ajili ya kuwajengea uelewa zaidi.
Naibu Waziri Jafo amesema kuwa sheria hiyo imelenga kuokoa fedha nyingi zanazoelekezwa katika miradi mbalimbali pamoja na kuipunguzia serikali gharama katika manunuzi ya umma.
Amesema kuwa kuna baadhi ya Wakandarasi waliopewa zabuni za mabilioni ya shilingi wakati wakiwa hawana ofisi zinazotambulika hali inayosababisha ubadhirifu wa fedha kutoka kwa wakandarasi hao.



