Jumatano , 27th Sep , 2017

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga R.P.C Benedict Michael Wakulyamba, amepiga marufuku Vigodoro ndani ya jiji hilo kutokana na vitendo hivyo kuhamasisha uhalifu.

Akiongea ofisini kwake R.P.C Benedict amesema miongoni mwa viashiria vya uvunjivu wa amani ni Vigodoro, ambavyo vinatumika kukusanya vijana wenye umri mdogo wakijiandaa kufanya uhalifu.

“Miziki ya kigodoro ni miziki ambayo ukiangalia namna inavyochezwa na hata washiriki wake ni vijana ambao wanatumia kama sehemu ya maficho kwaajili ya kufanya uhalifu”, amesema R.P.C Benedict.

Hata hivyo Kamanda Benedict ameongeza kuwa hakutakuwa na ruhusa yoyote ya kufanya Vigodoro katika eneo lolote na wananchi wanatakiwa kulinda utamaduni kwa njia nzuri na sio miziki inayovunja maadili.