Jumanne , 29th Nov , 2016

Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli jioni ya jana (Novemba 28, 2016) alimuandalia dhifa ya kitaifa mgeni wake Rais wa Zambia Edgar Lungu iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia

Rais Dkt Magufuli akigonganisha glasi na mgeni wake Rais Edgar Lungu wa Zambia.

Dhifa hiyo iliyofana kwa kiasi kikubwa ilihusisha viongozi mbalimbali wa sasa na wastaafu, huku pia wakialikwa wafanyabiashara, watendaji wa serikali, viongozi wa vyama vya siasa, mabalozi na watu wengine mashuhuri kama inavyoonekana katika picha:-

Rais Mstaafu wa awamu ya Pili AlhajAli Hassan Mwinyi,Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Mstaafu wa Zanzibar Dkt. Amani Abeid Karume wakielekea kwenye dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa heshima ya Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Lungu katika ukumbi wa Ikulu jijini Dar es salaam usiku huu.

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein, Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa wakielekea kwenye dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa heshima ya Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Lungu katika ukumbi wa Ikulu jijini Dar es salaam usiku huu.

 

Rais Dkt John Pombe Magufuli na  Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Lungu katika ukumbi wa Ikulu kwa dhifa hiyo ya kitaifa aliyomwandalia mgeni wake Ikulu jijini Dar es salaam usiku huu.

 

Meza kuu ikiwa imesimama kwa Wimbo wa Taifa

 

 Rais Dkt Magufuli akimsindikiza mgeni wake Rais Edgar Lungu wa Zambia kusalimiana na viongozi mbalimbali

 

Rais Edgar Lungu wa Zambia akisalimiana na Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi. Kulia ni Naibu Spika Dkt Tulia Ackson

 

Rais Edgar Lungu wa Zambia akisalimiana na Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete

 

 Rais Edgar Lungu wa Zambia akisalimiana na Naibu Spika Dkt Tulia Ackson

 

 Rais Edgar Lungu wa Zambia akisalimiana na Spika Mstaafu Mhe. Pius Msekwa

 

Rais Edgar Lungu wa Zambia akisalimiana na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman

 

Rais Edgar Lungu wa Zambia akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba

 

Rais Edgar Lungu wa Zambia akisalimiana na Rais Mstaafu wa Zanzibar Dkt Amani Abeid Karume

 

Viongozi wa vikosi vya ulinzi na usalama pamoja na Mkuu wa Itifaki wa Zambia wakiwa wamesimama kwa wimbo wa Taifa 

 

Wageni waalikwa na viongozi wa vyama vya siasa

 

Baadhi ya mabalozi mbalimbali waliohudhuria

 

Mrisho Mpoto na Banana Zorro na Mjomba band akitumbuiza

 

Rais Dkt. Magufuli, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Rais Mstaafu Dkt.  Jakaya Mrisho kikwete na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi wakifurahia jambo mara baada ya dhifa hiyo ya Kitaifa Ikulu jijini Dar es salaam. 

 

 Wafanyabiashara na viongozi wa taasisi mbalimbali na maafisa wa Wizara ya Mambo ya nje

 

Wafanyabiashara na viongozi wa taasisi mbalimbali