Mjiandae kuondoka - Waziri Mwijage

Thursday , 18th May , 2017

Waziri wa Viwanda, Mh. Charles Mwijage jana bungeni wakati akisoma bajeti ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji alitoa onyo kwa watumishi wote ambao wapo chini yake na kusema endapo wataruhusu bidhaa feki kuingia nchini wajiandae kuondoka.

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Bw. Charles Mwijage.

Mwijage alitumia nafasi hiyo kupiga marufuku bidhaa feki kuingia nchini kuanzia mwezi Julai 1 mwaka huu na kudai endapo zitaingia basi viongozi waliopo chini yake wajiandae kupisha ofisi zao.

"Tufikapo Julai 1 mwaka huu bidhaa zilizofeki zikipita mtakuwa hanitakii mema lakini na waliopo chini yangu mkae kabisa tayari mkao wa kuondoka kama bidhaa zisizokidhi viwango zitapita na kuja kuumiza viwanda vyetu chini" alisema Mwijage.