Alhamisi , 25th Apr , 2024

Kama alivyo Jean Claude Vandamme, Rambo, Arnold Schwarzenegger, Chuck Norris, Jackie Chan na Jet Li kuwa mastaa wa filamu za Action ndio hivyohivyo kwenye Game ya Muziki wa BongoFlava starring wake ni Masta AY Tanzania.

Picha ya AY kulia na Mr II Sugu kushoto

Jina lake linajiuza kimuziki tu kwa miaka 23 sasa na sio kiki, drama, skendo au bifu ameacha kazi zake kuongea zaidi.

U-Starring wake kimuziki ni wa vitendo sio kuforce, Ni msanii wa kwanza kuwekwa kwenye Category 1 na wasanii wakubwa duniani kama Jay Z na Kanye tuzo za MTV Base 2009.

Msanii wa kwanza kurekodi video nje ya mipaka ya Tanzania na video za nyimbo zake kuchezwa katika vituo vikubwa vya muziki Africa.

Ametengeneza soko la muziki wa BongoFleva kimataifa, amekuwa daraja la kusaidia wasanii wengi wa Bongo kufika level ile ya Kimataifa, amesaidia Collabo za wasanii wa nje na ndani kufanyika na kupendekeza majina yao na kazi zao kwenye tuzo kubwa za Africa.

Ameshaimba kuhusu nyimbo za bata (Leo, Cheza bila kukunja goti, Raha tu) ameiambia wanawake (Madem watafutaji) za kuelimisha maisha (Safari, Machoni kama watu, binadamu, I Don't Wanna be Alone) za Mapenzi (Yule, Ahsante na Zigo) mpaka zile za Commercial.

Kwa Ustarring wake huo Deiwaka Joseph Mbilinyi 'Mr II Sugu' akaona AY ni mtu muhimu sana kwenye Industry ya Muziki wa BongoFlava akasema Ijumaa hii ya April 26 jina lake linafaa kupewa heshima ya BongoFlava Honors.

Ni hayo tu tunayoyakumbuka kutoka kwa Starring huyu wa muziki wa BongoFlava. Tunakutana pale Ware House Masaki kwa kufanya Bonge Moja la Show na Surprise kibao kutoka kwa washkaji zake.