Alhamisi , 25th Apr , 2024

Ni headlines zingine za rapa Kanye West akifanya Interview na 'The Download Show with Justin La Boy' ambapo amekufuru kwa kujiita yeye ni Mungu anaiendesha dunia.

Picha ya Kanye West

"Sisi ni ufalme na mimi ndio Mkuu/kiongozi wa Ufalme. Mimi ni Mungu hakuna mtu anayeweza kutoa juu ya hilo mwisho. Mimi ni Mungu ninaendesha dunia" amesema Kanye West

Kupitia Interview hiyo amefunguka issues nyingi kama za kumpiga ngumi mtu aliyemshika mke wake, muziki wake, Bifu za wasanii zinazoendelea Marekani (Drake, Kendrick Lamar, J Cole) na Biashara zake.

Hii sio mara ya kwanza Kanye West kujiita Mungu, kupitia Album yake ya 6 'Yeezus' iliyotoka mwaka 2023, ipo ngoma inayoitwa 'I Am A God' akijifananisha na Mungu.