Jumapili , 21st Apr , 2024

Unaambiwa vita ya maneno kati ya Chris Brown na rapa Quavo limeifikia pabaya baada ya kutambiana kuchukuliana wapenzi wao wa zamani.

Picha ya Chris Brown na Quavo

Bifu limeanza Chris Brown kumpiga dongo Quavo kupitia ngoma yake ya 'Freak' baada ya ukaribu wa mpenzi wake wa zamani Karrueche Tran na Quavo ambao inasemekana wawili hao wapo penzini.

Diss ya Chris Brown kwa Quavo inasema "Kutembea na mpenzi wangu wa zamani haijafanya tuwe sawa kwa sababu sifanyi kama Cuervo (Quavo). Anapenda Casamigos sio Migos".

Quavo akamjibu Chris Brown kupitia ngoma ya Tender akisema "Umemfanyia vibaya na sasa ameenda. Amepost akiwa na Thug hata umpigie simu hatarudi nyumbani, usimpige, lazima itakuwa ni madawa".

Chris Brown akamjibu tena Quavo kupitia ngoma ya 'Weaklest link' akiimba "Umetembea na EX wangu sawa, kwa sababu nimetembea na EX wako wakati mkiwa wote penzini".

Ikumbukwe Karrueche Tran na Chris Brown walianza kudate 2011 mpaka 2015 walipoachana.

Ukiachalia mbali vita ya maneno ya Breezy na Quavo bifu lingine linalotrend Marekani kwa sasa ni Drake dhidi ya Rick Ross na Kendrick Lamar.