Ijumaa , 26th Apr , 2024

Mama lishe 50 kutoka Jiji la Arusha wamepewa mafunzo maalu na Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) kwa kushirikiana na Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA), kwa lengo la kuwaelimisha namna ya kukabiliana na majanga mbalimbali ya moto.

Mratibu wa idara ya dharura (ERT) kutoka GGML, Mohamed Mwaimu akimuonesha mama lishe namna ya kuzima moto wakati inatopokea mtungi wa gesi unapopata hitilafu na kulipuka. Mafunzo hayo yametolewana GGML kwa kushirikiana na OSHA kwa akina mama lishe 50 wa mkoani Arusha.

Mbali na mafunzo hayo, pia GGML imewagawia mitungi 50 ya gesi ya kupikia kwa ajili ya kuhamasisha akina mama hao kuachana na matumizi ya kuni na mkaa kisha kuhamia kwenye matumizi ya nishati safi.
 
Mafunzo hayo yalitolewa jana katika maadhimisho ya Kimataifa ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi yanayofanyika Kitaifa Jijini Arusha kuanzia tarehe Aprili 23 hadi Mei Mosi 2024.
 
Akizungumza na akina mama lishe hao, Meneja Mwandamizi wa Afya, Usalama na Mazingira kutoka GGML, Dk Kiva Mvungi alisema wamemua kutoa elimu kwa akina mama hao ili watambue namna ya kupambana na moto majumbani na kuzingatia usalama kwenye maeneo yao ya biashara hasa ikizingatiwa wao ni chanzo kikubwa cha kukutana na watu wengi.
 
“Tunawafundisha namna ya kupambana na majanga ya moto kwani shughuli zao  za kila siku zinahusiana na masuala ya moto na matumizi ya mkaa na gesi.
 
“Lakini pia ni vema kutambua namna gani mabadiliko ya tabia nchi yanaathiri watu pia namna tabia zetu binafsi zinavyoweza kuchangia kuachana na ukataji hovyo wa miti,” alisema.
 
Alisema athari za mabadiliko ya tabia nchi, zinamuathiri kila mmoja bila kujali, cheo, mkubwa au mdogo hivyo ni vema kila mmoja kuzingatia matumizi ya nishati safi ili kuondokana na majanga yatokanayo na mabadiliko hayo.
 
“Tumeandaa elimu hii kuona namna ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi kwa sababu ukataji wa miti ukikithiri unasababisha mmonyoko wa ardhi, mafuriko na ongezeko la joto duniani.
 
“Matumizi ya mkaa au kuharibu vyanzo mbalimbali ambavyo vinaweza kusabababisha athari kwenye mazingira na kusababisha mafuriko hata kwenye maeneo yetu ya uchimbaji,” alisema.
 
Naye Ofisa Mwandamizi wa masuala ya jamii na maendeleo ya kiuchumi kutoka GGML, Ruth Mharagi alisema katika mafunzo hayo, wamewafundisha akina mama hao namna salama ya kutumia nishati ya gesi na kuwasisitiza kuondokana na matumizi ya mkaa.
 
“Lakini pia kwenye banda letu tumeendelea kupokea wageni wanaopenda kujifunza namna ya kupambana na majanga ya moto kwa sababu asilimia kubwa wanauelewa mdogo namna ya kukabiliana na majanga ya moto majumbani,” alisema na kuongeza;

1.Mratibu wa idara ya dharura (ERT) kutoka GGML, Mohamed Mwaimu akiwaonesha mama lishe namna ya kuzima moto wakati inatopokea mtungi wa gesi unapopata hitilafu na kulipuka. Mafunzo hayo yametolewana GGML kwa kushirikiana na OSHA kwa akina mama lishe 50 wa mkoani Arusha.