Rais wa FIFA Gianni Infantino (Prestianni vs Vinicius Jr)
Chini ya mwongozo mpya uliopitishwa na bodi ya sheria za soka (IFAB), sasa mchezaji anaweza kuonyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja iwapo atafunika mdomo wake wakati anabishana au kurushiana maneno na mchezaji wa timu pinzani. (Mfano: Prestianni vs Vinicius Jr)
Mabadiliko hayo yanalenga kuzuia matumizi ya lugha chafu au ubaguzi ambayo mara nyingi hufichwa nyuma ya mikono ili isionekane na waamuzi au kamera za uwanjani.
Aidha, sheria hizo mpya hazitaishia hapo, kwani mchezaji yeyote atakayeamua kuondoka uwanjani kama ishara ya kugoma au kupinga uamuzi wa mwamuzi atajikuta akitolewa nje kwa kadi nyekundu mara moja.
FIFA imesisitiza kuwa kanuni hizo zimekuja ili kuhakikisha waamuzi wanapata udhibiti kamili wa mchezo na kupunguza vitendo vya utovu wa nidhamu ambavyo vimekuwa vikishika kasi katika soka kwa sasa.


