Ijumaa , 26th Apr , 2024

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amesema kuwa watu wasije wakashangaa ifikapo 2030 Mkuu wa Mjaeshi (CDF) akwa mwanamke.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan

Kauli hiyo ameitoa hii leo Aprili 26, 2024, jijini Dar es Salaam, wakati wa madhimisho ya miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

"Niwapongeze vikosi vya ulinzi, tumeona tofauti ya jeshi kabla ya Muungano lakini na vikosi vyetu vilivyopita hapa leo, lakini kwa namna ya pekee katika miaka 60 yote tumezoea kuona kikosi cha bendera kina wanaume watupu leo kikosi cha bendera kina mwanamke na huo ndiyo mwanzo wa safari mshije mkashangaa 2030 tuna CDF  mwanamke hapa," amesema Rais Samia.

Aidha Rais Samia akizungumzia uchumi amesema, "Leo hii tunayo fahari kuwa nchi yetu imefika hadhi ya uchumi wa kati ngazi ya chini na tathimini zote zinaonesha kuwa kuna mwelekeo mzuri wa kuimarika na kuweza kufikia uchumi wa kati ngazi ya juu, hivyo tuendelee kudumisha amani ya nchi yetu ili tuendelea kujenga uchumi wa nchi yetu,".