Mradi wa uwekezaji katika sekta ndogo ya gesi ni moja ya maeneo ambako wawekezaji wamekuwa wakitumia uelewa duni kukwepa ulipaji kodi.
Hayo yamebainika katika mkutano wa kamati ya umoja wa mataifa inayoshughulikia maswala ya kodi katika sekta za madini ,gasi na mafuta,ambapo lengo ni kuwa na uwiano wa utozwaji wa kodi kwa nchi zote zinazo endelea.
Nae mjumbe wa kamati ya utekelezaji inayosimamia mapato hapa nchini Aman Mustapha amesema wananchi wa nchi zinazokabiliwa na changamoto hizo wamekuwa na imani kubwa juu ya maliasili walizonazo, lakini kutokana na mfumo wa serikalia kufanya kazi na kampuni za nje bado wamekuwa hawanufaiki ipasavyo
Wakati huo huo, mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk, Rehema Nchimbi, amezitaka Halmashauri za Wilaya katika mkoa wa Dodoma kutenga maeneo maalum kwa ajili kuwawezesha vijana kufanyia shughuli zao za ujasiriamali.
Dk, Nchimbi, ametoa wito huo wakati akipokea mashine 28 za kufyatulia matofali kutoka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kwa ajili ya vikundi saba vya vijana kutoka katika Wilaya saba za mkoa wa Dodoma katika Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma.
Amesema ili kuwavutia vijana kujiajiri na shughuli hiyo ya ufyatuaji wa matofali ni lazima Halmashauri za Wilaya ziweze kuwasimamia na kuwapatia maeneo kwa ajili kuendeshea shughuli zao.