Rais Magufuli na Aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa Tabora Aggrey
Kwanza Rais Magufuli amemteua Dkt. Philemon Sengati kuwa mkuu wa mkoa wa Tabora, akichukua nafasi ya Mh Aggrey Mwanri ambaye amestaafu.
Pia Rais Magufuli amemteua Bw. Thobias Andengenye kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma akichukua nafasi ya Brigedia Jenerali Mstaafu, Emmanuel Maganga ambaye amestaafu.
Aidha Rais Magufuli amemhamisha kituo cha kazi aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Handeni Godwin Gondwe ambapo sasa anakwenda kuwa mkuu wa wilaya ya Temeke, akichukua nafasi ya Bw. Felix Jackson ambaye amestaafu.
Zaidi soma taarifa ya Ikulu hapo chini