Tume ya Uchunguzi wa Matukio ya Uvunjifu wa Amani Wakati na Baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, imependekeza Serikali itenge siku ya maombelezo ya kitaifa kuwakumbuka watanzania zaidi ya 500 waliofariki katika ghasia za wakati na baada ya uchaguzi mkuu.
Hayo yameelezwa leo Alhamisi Aprili 23, 2026, Ikulu jijini Dar es Salaam wakati wa kukabidhi ripoti kwa Rais Samia Suluhu Hassan, Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji mstaafu Mohamed Chande.
Pia, Jaji Chande amependekeza kwa Serikali kuweka mkakati wa utoaji wa huduma ya msaada wa kisaikolojia, matibabu kwa majeruhi na kufanyika kwa tathimini ya haraka katika maeneo yaliyoathirika.
“Majeruhi waliopata ulemavu kutokana na ghasia wapatiwe huduma za matibabu bure pamoja na wataohitaji vifaa saidizi ikiwa ni pamoja na viungo bandia,” amesema Jaji Chande.



