Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Awamu ya sita yadhamiria makubwa Shinyanga

Ijumaa , 15th Mar , 2024

Katika kipindi cha Miaka mitatu, Serikali  ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeunga Mkoa wa Shinyanga kwa miradi mbalimbali ya Ujenzi na ukarabati wa Miundombinu ya barabara na madaraja.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari leo Machi 10, 2024 kuhusu mafanikio kwa kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Dkt Samia Suluhu Hassan katika sekta ya ujenzi; Kaimu Meneja wa TANROADS Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Samweli Mwambugu amesema ndani ya muda huo Serikali kupitia Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) imeendeleza miradi mbalimbali Mkoani humo.

Amesema miradi minne ya Kitaifa inaendelea kutekelezwa ikiwemo upanuzi na Ujenzi wa Uwanja wa ndege wa Ibadakuli, Ujenzi wa barabara ya Mwigumbi - Lamadi kwa kiwango cha lami, Sehemu ya kwanza Mwigumbi-Maswa ( Km50.3), Ujenzi wa barabara ya Kagongwa-Bukoba - Nzega, (km 66) ambapo Km 11.3 zipo katika Mkoa wa Shinyanga pamoja na Ujenzi wa barabara ya Kahama - Kakola (Km 73) kwa kiwango cha lami.

Amesema pia kumefanyika upembuzi yakinifu na Usanifu wa kina kwa ajili ya kujenga kwa kiwango cha lami, barabara ya Kolandoto - Laiago ( Km 53), Salawe-Old Shinyanga( Sehemu ya Solwa-Old Shinyanga, 64.66), Uyogo - Nyamilangano-Nyandekwa - Kahama,  Km 54 zipo Shinyanga hadi Kaliua na Mpanda pamoja na barabara ya Old Shinyanga - Bubiki( Km 35).

Mhandisi Mwambugu ameishukuru Serikali kwa kutekeleza mradi wa kusimika jumla ya taa 395 katika Miji na vijiji vya Tinde, Isaka, Kagongwa, Kahama, Segese na Bulige ikiwa ni pamoja na taa nyingine zitakazofungwa maeneo ya Vijiji vya Solwa na Ngaya.

Ameeleza "Serikali imetoa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa Miradi ya maendeleo na matengenezo ya barabara kwa Mkoa wa Shinyanga  ili kufanya mtandao wa barabara uweze kupitika kipindi chote cha mwaka”.

Aidha Katika Miundombinu Mkoa wa Shinyanga unahudumia mtandao wa barabara zenye jumla ya Km 1,177.74 na Madaraja 309, kati ya Km 1,177.74 barabara za lami ni Km 261.102 na barabara za Changarawe ni Km 916.72.

HABARI ZAIDI

Baadhi ya Wakazi wa Kata ya Madanga Mkoani Tanga

Wagoma kubeba mimba kwa kukosa huduma za afya

Mkuu wa mkoa wa Songwe Daniel Chongolo

Wanafunzi 194 washika mimba ndani ya mwezi mmoja

Mabaki ya gari aina ya Noah iliyopata ajali Morogoro

Ajali yachukua uhai wa watu saba Morogoro

Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba

Wawekezaji wawekeze sekta za uzalishaji - Nchemba

Muonekano wa Kiburugwa ambako Nyumba zaidi ya Tisa Zimebomolewa na Maporomoko ya Tope

Maporomoko ya udongo yasomba nyumba 9 Mbagala

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko

Serikali yaipongeza Red Cross

Waziri wa TAMISEMI Mohamed Mchengerwa

Aonya wanaochangia watumishi kutopanda madaraja