Jumanne , 22nd Oct , 2024

Watu watano ambao ni wanakwaya wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) wamefariki Dunia na wengine 20 kujeruhiwa baada ya gari walilokuwa wakisafiria kuacha njia na kuingia kwenye daraja.

Kwa mujibu wa Mkuu wa wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni (Pichani) amesema usiku wa kuamkia leo majira ya saa tisa usiku gari aina ya Costa iliyokuwa imebeba Wanakwaya wakitokea jijini Dar es salaam kuelekea Machame ilipofika eneo la Kirinjiko wilayani Same liliacha njia na kusababisha vifo hivo.

Mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa, uchunguzi wa awali unabainisha kuwa Dereva wa gari hilo alisinzia na kupelekea gari hilo kuacha njia na kuingia kwenye daraja.

Alisema kuwa, kwa sasa majeruhi wanatibiwa katika hospitali ya wilaya ya Same. #EastAfricaTV