Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

23 mahakamani tuhuma biashara ya dawa za kulevya

Jumatano , 13th Mar , 2024

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini (DCEA) kwa kushirikiana na Ofisi ya Taifa ya Mashitaka (NPS) wamewafikisha katika Mahakama ya wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga watu 23 wanaotuhumiwa kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya.

Watuhumiwa biashara ya dawa za kulevya

Watuhumiwa wamefikishwa mbele ya Mahakama hiyo kujibu tuhuma za kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya aina ya bangi, heroin na mirungi kinyume cha sheria ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya sura 95 marejeo ya mwaka 2019 kifungu cha 15 A kifungu kidogo (1) (2) na kifungu cha 17. 

Akisoma mashauri hayo 18 ya jinai mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo Christina Chovenye, Wakili wa Serikali John Hamenya alisema kuwa watuhumiwa hao walitenda makosa hayo kwa nyakati tofauti katika mwezi Februari na Machi mwaka 2023 katika wilaya ya Kahama huku wakijua wazi kuwa biashara hiyo ni kosa kisheria.

Watuhumiwa wote kwa pamoja wamekana mashtaka yanayowakabili na mashauri yao yameahirishwa hadi Machi 14,15 na 26 mwaka huu kwa hatua ya kutajwa na kusikilizwa baada ya upelelezi kukamilika. 

Hamenya amewataja watuhumiwa hao 23 ambao wamefikishwa mahakamani kuwa ni, Juma Lusangija (54), Mwajuma Kavula(36), Tayson Mwita Marwa (23) Emmanuel Christopher (33), Amos Augustino 34, wakazi wa mtaa wa Mwime na Fred Bichuka(37) , Rojasi Daudi (18) wakazi wa mtaa wa Mhungula na Juma Merengo Merena (44) mkazi wa Kidete , Hassan ally Ngwenyau (27) mkazi wa Nyakato na Gerald Emmanuel (18) mkazi wa Nyasubi.

Wengine ni pamoja na Paulo Charles Wilson (25) Nyakato, Joseph Lugenzi, Zamoyoni Andrea (26) mkazi wa Nyashimbi , Kobelo Ntahondi(42) Mkazi wa Bukondamoyo, Raphael Masanja (37) mkazi Nyakato na Said Kayoka kayoka (27) mkazi wa Mhungula, Saidi mselem (22) mkazi wa Majengo, na Haitham salum Suleiman (31) mkazi wa Nyasubi. 

Samwel Edward John (31) mkazi wa Malunga, Joseph Mussa lugenzi,(40) mkazi wa Malunga, Robert Elias Lameck (24) mkazi wa Mwitongo , Hillary salum nassoro(39) mkazi wa Malunga ,Richard Raphael mushi (30) mkazi wa Majengo, Izdory Nemes temba(23) mkazi wa Malunga, Kassim hamad amori(27) mkazi wa Nyasubi.

Hata hivyo, nafasi ya dhamana kwa watuhumiwa iko wazi kwa Watakaokidhi vigezo vya Mahakama.

HABARI ZAIDI

Baadhi ya Wakazi wa Kata ya Madanga Mkoani Tanga

Wagoma kubeba mimba kwa kukosa huduma za afya

Mkuu wa mkoa wa Songwe Daniel Chongolo

Wanafunzi 194 washika mimba ndani ya mwezi mmoja

Mabaki ya gari aina ya Noah iliyopata ajali Morogoro

Ajali yachukua uhai wa watu saba Morogoro

Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba

Wawekezaji wawekeze sekta za uzalishaji - Nchemba

Muonekano wa Kiburugwa ambako Nyumba zaidi ya Tisa Zimebomolewa na Maporomoko ya Tope

Maporomoko ya udongo yasomba nyumba 9 Mbagala

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko

Serikali yaipongeza Red Cross

Waziri wa TAMISEMI Mohamed Mchengerwa

Aonya wanaochangia watumishi kutopanda madaraja