Mzee Juma Kankaa afariki dunia
Aliyekuwa msanii mkongwe wa maigizo hapa nchini, Mzee Juma Kankaa amefariki dunia alfajiri ya leo nyumbani kwake huko Tandale baada ya kusumbuliwa na maradhi ya kiharusi na vilevile majeraha ya kugongwa na gari, tukio lililomkuba mapema mwaka jana.