Tuesday , 23rd Jun , 2015

Korti ya Manzese imeamuru mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu akabidhiwe mtoto wao Sasha Desderia kumlea, kufuatia kesi aliyofungua dhidi ya mke wake wa zamani Faiza Ally.

Sugu na mwanae Sasha

Maamuzi hayo yamefikiwa baada ya Sugu kulalamikia maadili ya mama wa mtoto huyo, akihofia kuharibika kwa mwanaye, kigezo dhahiri kikiwa ni picha za vivazi tata ambavyo mwanadada huyo amekuwa akionekana navyo na pia kuweka mtandaoni.

Hata hivyo mambo yanaonekana kuwa bado ni moto kwa upande wa shauri hilo baada ya Faiza kuweka wazi nia yake ya kukata rufaa kwa madai kuwa mwanae huyo bado ni mdogo sana na anahitaji kuwa karibu na mama yake.