Jumatatu , 1st Jun , 2026

Aliyekuwa kocha mkuu wa kikosi cha Liverpool Arne Slot alisema mashabiki walimsaidia kukiongoza kikosi cha Liverpool katika kipindi cha misimu miwili huku akidai hana mashaka na kikosi alicho kiacha.

Arne Slot

"Ninaondoka nikiwa na imani kamili katika kile kilicho mbele, Wachezaji ambao wamejitolea sana kwa klabu hii, ambao wamedumisha maadili yake na kusaidia kuunda nyakati nyingi zisizosahaulika, wamejenga misingi ambayo itadumu."

Licha ya matokeo mabovu katika msimu uliopita lakini Slot aliihakikishia klabu hiyo nafasi ya kushiriki katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya kwa msimu ujao

"Kuhakikisha soka la Ligi ya Mabingwa ilikuwa jukumu muhimu na linalohakikisha Liverpool inaweza kuendelea kushindana katika kiwango cha juu zaidi msimu ujao na zaidi," 

"Mabadiliko ni sehemu ya mpira wa miguu, lakini najua kwamba klabu hii itaendelea kuwafanya watu wake wajivunie, Niliposimama chini ya bango hilo kwa mara ya kwanza kwenye handaki la Anfield, nilijua kile klabu hii ilichohitaji. Ninaondoka nikijua hatujawahi kuacha kujitahidi kukipata." - Slot