Azam FC kuwakosa Wanga, Balou mechi ngao ya Jamii
Timu ya Azam FC imesema inaendelea na maandalizi isipokuwa itamkosa Kipre Michael Balou kutokana na kuwa majeruhi pamoja na Allan Wanga ambaye bado yupo kwao kwa ajili ya kuhudhuria mazishi ya mama yake yanayotarajiwa kufanyika Agosti 22.

