TFF yashukuru wadau kwa mapokezi ya Samatta
Shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF limewapongeza wanamichezo,wadau,na wananchi kwa ujumla kwa mwitikio wao wa kujitokeza kwa wingi katika kumlaki na kumpokea Mbwana Samatta kwa kushinda tuzo ya mchezaji bora wa ligi za ndani Afrika.