Rungu la TFF lawashukia watovu wa nidhamu
Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi imeipiga faini ya sh. 500,000 (laki tano) klabu ya Stand United baada ya timu yake kupata kadi zaidi ya tano kwenye mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom dhidi ya Coastal Union iliyofanyika mkoani Tanga.

