Mauaji yanayoendelea nchini lazima yakomeshwe
Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Kamishna Diwan Athuman, amesema watanzania washirikiane vema na jeshi la Polisi katika kutoa taarifa za kuwafichua wote wanaotenda ukatili wa mauaji ili hatua kali za kisheria zichukuliwe dhidi yao.